Mgombea wa urais wa Fifa mwana mfalme Ali bin al-Husein
Mwana mfalme Ali, mwenye umri wa miaka 40, amesema hafurahishwi na mipango ya upigaji kura na amewasilisha kesi yake kwa mahakama ya kutatua maswala ya michezo.
Mgombezi huyo kutoka Jordan, aliomba sehemu za kupiga kura kuwa za uwazi , ombi ambalo tume ya kimataifa ya uchaguzi wa soka limepinga.
Ali ni mmoja wa wagombea wengine watano wanaotaka kumrithi Sepp Blatter, ambaye anang'atuka mamlakani baada ya miaka 18 tangu mwaka 1998.
Licha ya nguvu yake kiongozi huyo anakabiliana na upinzani kutoka kwa Jerome Champagne, Gianni Infantino, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa na Tokyo Sexwale katika kinyang'anyiro cha kuwania urais wa FIFA.




