Paul Pogba
Magazeti mengi ya michezo nchini Italia yamechapisha habari hiyo kwenye ukurasa wa kwanza kuwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23 ameomba aruhusiwe kuondoka kwani posho ya Man United inavutia.
Gazeti la 'La Gazzetta dello Sport' liliongoza na kichwa cha habari kinachosomeka ''Pogba ameamua kuondoka Juventus''.
Gazeti hilo linadai kuwa mfaransa huyo amekwisha kubaliana ya mashetani wekundu huku likisisitiza kuwa sababu kuu iliyomfanya makamu wa mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Ed Woodward asiongozaje na timu ya Manchester united kwenda China ilikuwa ni kwa sababu alikuwa ameamua kuandaa ombi rasmi la kumsajili mchezaji huyo wao wa zamani.
Iwapo mkataba huu utafaulu, mfaransa huyo ndiye atakayekuwa mchezaji aliyegharimu kitita kikubwa zaidi cha fedha katika historia ya kandanda.
Chanzo BBC




