Saturday , 3rd Nov , 2018

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Emmanuel Amunike, ametaja kikosi cha wachezaji 27 kitakachoingia kambini kujiwinda na mchezo wa kufuzu fainali za AFCON 2019, dhidi ya Lesotho.

Wachezaji wa Taifa Stars kwenye mazoezi.

Mchezo huo ambao ni wa kufa na kupona kwa Taifa Stars utapigwa Novemba 18, 2018 Mjini Maseru, Lesotho. Stars ina alama 5 katika nafasi ay pili kwenye Kundi L lenye timu za Uganda, Lesotho na Cape Verde.

Katika majina hayo 27 Amunike ameita wachezaji 8 wanaokipiga soka la kulipwa nje ya Tanzania akiwemo nahodha Mbwana Samatta ambaye kwasasa ni kinara wa mabao katika ligi kuu ya soka nchini Ubelgiji.

Wachezaji wengine kutoka nje ni Simon Msuva anayechezea Diffaa El Jadidi ya Morocco, Shabani Chilunda wa Tenerife ya Hispania, Hassan Kessy wa Nkana Rangers ya Zambia, Thomas Ulimwengu wa Al Hilal ya Sudan na Rashid Mandawa wa BDF ya Botswana, Abdi Banda wa Baroka FC na nahodha msaidizi Himid Mao wa Petrojet ya Misri.

Kwa upande wa vilabu vya Tanzania, Simba wamekuwa vinara kwa kutoa wachezaji 6 huku Azam FC ikitoa wachezaji 5 na Ynaga ikitoa nyota 4 ambapo kati yao hakuna jina la Ibrahim Ajibu ambaye ndiye kinara wa kutoa msaada wa mabao kwenye ligi kuu akifanya hivyo mara 7.

Orodha kamili kama inavyoonekana hapo chini.