Monday , 11th Jul , 2016

Machozi na hisia kali baada ya kuumia mapema katika fainali ya Mataifa ya Ulaya, kisha kutolewa nje dakika ya 25, kulimfanya Cristiano Ronaldo kuwa kocha msaidizi nje ya uwanja wakati akiwahamasisha wachezaji wenzake wa Ureno kuiangamiza Ufaransa.

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo amesema alikuwa na kiu ya muda mrefu kutwaa taji la Mataifa ya Ulaya, baada ya hapo jana kucheza kwa dakika 25 na kutolewa nje kwa kuumia, wakati timu ya Taifa lake ikichukua taji hilo kwa mara ya kwanza usiku wa jana, huko Paris, Ufaransa.

Nyota huyo wa Real Madrid, alisema " Nina furaha sana, nimesubiri kwa muda mrefu tangu 2004.Nilimwomba mungu kwa nafasi nyingine.

Ureno iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ufaransa, kwenye uwanja wa Stade de France, jijini Paris.