Dereva Nico Rosberg katika picha
Kwa mujibu wa timu ya Marcedes ni kwamba Rosberg ambaye kwa sasa ndiye kinara wa Formula one ameridhia mkataba huo na sasa ataendelea kufanya kazi na mwenzake Lewis Hamilton kwa muda mrefu zaidi.
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka thelasini na moja amekua na mwenendo mzuri ndani ya timu hiyo ambapo kwa msimu miwili mfululizo amemaliza nafasi ya pili nyuma ya bingwa Lewis Hamilton.
Ikumbukwe mnamo mwaka jana mwezi mei bingwa mara mbili wa formula one Lewis Hamilton alisaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo ambao pia utamalizika mwaka elfu mbili na kumi na nane.






