
Saimon Msuva
Saimon Msuva ameyasema hayo baada ya mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Stade De Bommel Mjini Moroni katika kisiwa cha Comoro.
"Kwanza tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa matokeo tuliyopata, tulicheza katika uwanja ambao ni artificial hatukutegemea kama ndiyo uwanja ambao tunaweza kuchezea kwani ni mzuri, ila tu mazingira hayakuwa mazuri sana lakini tumeweza kupambana, tumeweza kuwakilisha Tanzania sababu hii siyo Yanga tu hivyo tumeiwakilisha Tanzania kama Tanzania, tunashukuru kwa watu wote walioweza kufika hata wale ambao walishindwa kufika tunashukuru kwa support yao". Alisema Saimon Msuva
Mbali na hilo Simon Msuva anasema ushindi wao huo wameutoa kama zawadi kwa Mwenyekiti wao kutokana na matatizo anayopitia na kusema wao kama wachezaji hawajayafurahia.