Tuesday , 19th Jun , 2018

Kuelekea michuano ya klabu Bingwa Afrika mashariki na kati (KAGAME), mshambuliaji mpya wa Azam FC Donald Ngoma, imethibitika kuwa hataweza kushiriki michuano hiyo kutokana na kutokuwa vizuri kwa sasa.

Taarifa kutoka Azam zinaeleza kuwa Ngoma atakuwa nje ya uwanja katika mechi za ushindani mpaka mwezi August mwaka huu ndipo atakaporejea dimbani rasmi tayari kwa mapambano.

Mshambuliaji huyo aliyetoka Yanga na kujiunga na matajiri hao, alipelekwa Afrika ya Kusini kuangaliwa vizuri afya yake kutokana n kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu alipokuwa akikitumikia kikosi cha Yanga.

Aidha kwa upande mwingine Azam wamethibitisha kuwa, kuelekea michuano hiyo Tafadhwa Kutinyu, Mudathit Yahaya na wengine wote waliosajiliwa watakuwa tayari kushiriki ili kuhakikisha wanatetea ubingwa wao.

Azam FC ndio mabingwa watetezi wa michuani hiyo ambayo waliutwaa ubingwa huo miaka mitatu iliyopita huku Tanzania ikiwakilishwa na Azam FC pamoja na Simba huku Yanga wakijitoa katika mashindano hayo