Kocha wa klabu ya Valencia Garry Neville (pichani)ameiongoza Valencia kwenye mechi ya ushindi dhidi ya Las Palmas jana.
Bao pekee na la ushindi la Valencia lilifungwa na nyota wa zamani Bolton Wonderes Rodrigo ndilo lilowapa ushindi vijana wa kocha Garry Neville kuvuka hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye mechi zote mbili.
Neville raia wa Uingereza alichukua mikoba ya umeneja klabuni hapo mwezi Disemba mwaka jana na ameingoza kwenye mechi nne za ushindi kwenye michuano ya kombe la mfalme.
Licha ya ushindi huo Beki huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United bado anasaka ushindi wa kwanza wa ligi kuu nchini Hispania.
Nayo klabu ya Sevilla imetinga nusu fainali kufuatia ushindi wa jumla wa bao 5-0 baada ya hapo jana kuinyuka Mirandess bao 3-0 .
Sevilla na Valencia zimeungana na Celta Vigo na mabingwa watetezi Barcelona kusubiri ratiba ya nusu fainali inayotarajiwa kupangwa hii leo.


