Wednesday , 13th Jul , 2016

Klabu ya soka ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara imetangaza kuachana na wachezaji wake watatu ambao walikuwa nao katika misimu miwili iliyopita katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kikosi cha Ndanda FC kilichoshiriki ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2015/16

Akizungumza na Kipenga cha East Africa Radio, afisa habari wa klabu hiyo Idrissa Bandari, amewataja wachezaji hao kuwa ni viungo, Omega Seme, Asili Mnkondya pamoja na Masoud Ally ambao mwalimu Malale Hamsini amependekeza kutowaongezea mikataba kwa ajili ya kuwatumia msimu mpya wa ligi.

Aidha, Bandari amesema zoezi la usajili linaendelea vizuri ambapo kwa sasa wanapambana kuhakikisha wanawaongezea mikataba wachezaji wao pamoja kuwaongeza wengine wapya licha ya kuondokewa na baadhi mshambuliaji Atupele Green na Kassian Ponera aliyetimkia Mtibwa Sugar, huku akiipongeza kampuni ya Azam Media kwa kuongeza mkataba wa udhamini ambao unataraji kuleta changamoto kubwa ya ushindani.

Timu hiyo imepanga kusajili wachezaji wasiozidi 25 msimu huu ambao wanaamini watatosha kumudu mikikimikiki ya ligi kuu msimu mzima.

Msikilize hapa Idriss Bandari....

Sauti ya Idriss Bandari akielezea sababu za kuachana na wachezaji hao
Sauti ya Idriss Bandari akielezea mipango ya usajili mpya