Wednesday , 1st Jul , 2015

Mshindi namba tisa wa mbio za nyika za Dunia, Ismail Juma amepata mualiko wa kushiriki mashindano ya Riadha ya kimataifa yanayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu nchini China.

Katika taarifa yake Ismail amesema, mashindano hayo yatashirikisha wanariadha maarufu duniani na anatarajia kukimbia mbio za nusu Marathon ambazo ni Kilomita 21 na Kilomita tisa ili kutafuta viwango vya kufuzu mashindano ya Dunia na All African Games.

Ismail amesema, katika maandalizi ya mashindano hayo ambayo hufanyika Agosti kila mwaka, anafanya mazoezi ya peke yake wilayani Babati mkoani Manyara kwa kufuata Programu aliyoandaliwa na mwanariadha wa zamani wa mita 10,000 Zacharia Barie.