
Mtendaji mkuu wa Bodi ya ligi Silas Mwakibinga amesema, kuwa hana shaka kwa uwanja wa jamhuri ambao utatumiwa na pilisi Morogoro kwani uwanja huo unatumika hivi sasa kwa michezo ya ligi kuu na klabu vya Mtibwa sugar
Aidha Mwakibinga amesema, mfano uwanja wa umoja kule Mtwara ambao hivi sasa unajulikana kama Nangwanda, nao unahitaji marekebisho madogo ili uweze kifikia kiwango cha kuchezewa ligi kuu.
Hali kadhalika uwanja wa Kambarage Shinyanga, Mwakibinga amesema nao pia ufanyiwe marekebisho, kwakuwa kuna uwezekano wa moja ya timu kati ya Stand united au Mwadui ikapanda ligi kuu msimu ujao.
