Sunday , 13th Mar , 2016

Mtibwa Sugar imeibuka na pointi tatu za Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa JKT Ruvu mabao 2-1 Uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro.

Kikosi cha Mtibwa Sugar

JKT iliyochini ya Kocha mkongwe nchini, Abdallah King Kibadeni, imezidi kudidimia na sasa imeendelea kubaki na pointi 21 wakiwa katika hatari ya kushuka daraja.

Katika mechi hiyo, Mtibwa ndiyo wa kwanza kupata bao kupitia beki wake Salim Mbonde katika dakika ya 9 na Shiza Kichuya akaongeza la pili katika dakika ya 22.

JKT walipata bao lao katika dakika ya 24 kupitia kwa Saad Kipanga na mapumziko ikawa 2-1.

Katika kipindi cha pili, Mtibwa walitaka kuongeza bao, JKT wakataka kusawazisha lakini hakuna timu iliyofanikiwa kubadili matokeo hayo na kapelekea Dakika 90 kumalizima Mtibwa akiwa anaongoza bao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu.