Friday , 4th Dec , 2015

Mshindi wa shindano la East Africa Radio Fantacy League Frank Mugoyoko amekabidhiwa zawadi yake ya kitita cha shilingi milioni moja za kitanzania hii leo katika ofisi za East Africa Radio zilizopo mikocheni jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi yake Mukoyoga amewashukuru waandaaji wa shindano hilo kwa kutoa fursa kwa watanzania na wengineo kwa ujumla kupata nafasi ya kushiriki bure na kujishindia zawadi hiyo.

Mugoyoka amewaasa wananchi kusikiliza East Africa Radio ili wajue kinachoendelea ili wajue namna ya kushiriki shindano hilo ambalo mwisho wa siku mshindi wa jumla atazawadiwa milioni 10.

katika makabidhiano hayo mshindi huyo alizawadiwa mpira na kaimu mkuu kitengo cha masoko kutoka benki ya Barclays Joe Bendera.

Makabidhiano ya fedha hizo yaliendana sambamba na hafla ya kupokelewa kwa kombe la Barclays Premier League hii leo kwenye ofisi za East Africa Radio ambalo lipo kwenye ziara hapa nchini kabla ya kurejea nchini Uingereza.