Bondia Francis Cheka akipongezwa katika moja ya mapambano aliyoshinda ubingwa
Bondia Gavad Zohrevand toka nchini Iran ambaye aliwasili nchini jana jioni hii leo amefanya mazoezi katika gym ya Rio tayari kumkabili bondia Mtanzania Francis Cheka SMS katika mpambano mkali wa dunia uzito wa juu mwepesi yaani light heavy weight kilo 81.
Bondia huyo ambaye amewahi kutwaa ubingwa wa bara la Asia asema pambano lake na Cheka litakua gumu kwakua amemwangalia Cheka katika video na kubaini hilo na hivyo amejipanga kuibuka na ushindi siku hiyo ya Jumamosi ya Aprili 12 watakapopanda ulingoni kuoneshana uwezo.
Kwa upande wake mratibu msaidizi wa pambano hilo Jay Msangi amesema maandalizi ya mpambano huo yamekamilika na hivyo amemtaka bondia Francis Cheka ajipange vilivyo kumkabili bondia huyo kutoka nchini Iran kwani si wakumbeza.
