Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amekiri kuwa anataka kufunga usajili na mchezaji mmoja hivi karibuni, lakini akakataa kutaja jina la mchezaji huyo.
Mourinho, amesema dirisha la usajili linafungwa Agost 31, hivyo kuna muda wa kutosha kufanya usajili wa mwisho, ili kuwahi msimu mpya wa EPL.
Tunataka kusajili mchezaji mmoja, huo ndiyo ukweli."Sitaki kuzungumzia juu ya Paul Pogba, kwa sababu ni mchezaji wa Juventus, na sitaki makocha wengine wazungumzie wachezaji wangu. Amesema Mourinho.



