Friday , 30th Sep , 2016

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa amesema, hachukulii mchezo dhidi ya Ethiopia kama mchezo wa kirafiki pekee bali anakiandaa kikosi chake kupambana kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri ya viwango vya ubora vya FIFA

Mkwasa akiongoza mazoezi ya Taifa Stars

Mkwasa amesema ameita kikosi imara ambacho kitaingia kambini Oktoba 02 na kuanza mazoezi Oktoba 03 huku akiwaacha wachezaji ambao ni majeruhi ambao ni Thomas Ulimwengu pamoja na Shomari Kapombe na kuongeza wachezaji wengine wapya ili kuhakikisha kikosi kinaendelea kuwa imara zaidi kwa ajili ya mpambano huo.

Matokeo ya mchezo huo utakaopigwa Oktoba 09 mwaka huu nchini humo ni sehemu maalumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa ambapo kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora huku Ethiopia ikishika nafasi ya 126.