Franccis Miyeyusho akipambana katika moja ya mapambano yake na Mmalawi John Masamba.
Pambano la ngumi kati ya bondia Francis Miyeyusho 'Chichi Mawe' dhidi ya bondia Mohamed Matumla litapigwa Mei 10 mwaka huu kama lilivyopangwa katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, licha ya Miyeyusho kupigwa kwa KO na bondia Sukkasem keityongyuth kutoka Thailand katika pambano lililopigwa April 19 mwaka huu.
Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBO), Yasin Abdallah 'Ustaadh' amesema kupigwa kwa Miyeyusho kwa KO katika round ya kwanza hakumzuii kupanda ulingoni endapo ripoti ya daktari inaonyesha yuko fiti kupambana.
Ustaadhi anasema baadhi ya mabondia duniani ikiwa ni pamoja na Manny Paquiao na Mike Tyson walishapigwa katika mapambano yao katika mizunguko ya mwanzo ya mwanzo ya mapambano yao lakini waliendelea na masumbwi na kufanya vizuri.