Thursday , 10th Jul , 2014

Chama cha riadha Tanzania RT kimepongeza mwitikio wa mikoa katika ushiriki michuano ya mwaka huu ya taifa ya riadha itakayofanyika kwa siku mbili katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam

Wanariadha wa Tanzania wakichuana katika moja ya michuano ya taifa.

Timu 20 za mikoa zitakazoshiriki michuano ya taifa ya riadha zimethibitisha kushiriki michuano hiyo ambayo inataraji kuanza jumamosi Julai 12 hadi jumapili Julai 13 mwaka huu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam

Katibu mkuu msaidizi wa chama cha riadha Tanzania RT Omben Zavala amesema maandalizi yote yamekamilika na kesho waamuzi watafanya mazoezi ya vitendo katika uwanja wa taifa kwaajili ya kujiweka sawa kwa mashindano hayo ambayo pia wawakilishi wa Tanzania ya michuano ya jumuiya ya madola ambao walikua nje ya nchi katika kambi maalumu ya maandalizi ya michuano ya madola watashiriki kupima viwango vyao

Aidha Zavala amesema kiutawala wamekamilisha maandalizi yote ikiwemo suala la sehemu ya malazi kwa wachezaji, sehemu ya kupata chakula na masuala ya usafiri lakini bado RT inakaribisha wadau na wadhamini ili kusaidia mashindano hayo katika suala la kuongeza zawadi kwa washindi na kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa katika kiasi kikubwa kwani ndio mashindano ambayo yanatoa wachezaji ambao wanateuliwa katika timu za taifa ili kuwakilsha nchini katika michuano mbalimbali ya kimataifa.