Wednesday , 10th Feb , 2016

Klabu ya Zamalek ya nchini Misri imemtimua kocha wake Ahmed Hossam Hussein maarufu kwa jina la Mido kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo.

Klabu ya Zamalek ya nchini Misri imemtimua kocha wake Ahmed Hossam Hussein Abdelhamid maarufu kwa jina la Mido kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa Mido kuajiriwa na kutimuliwa katika klabu hiyo, ambapo safari hii amekinoa kikosi hicho kwa siku 37 pekee.

Mido ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Tottenham na Middlesbrough za England alipewa tena majukumu ya kukinoa kikosi hicho Januari nne mwaka huu na amekiongoza kushinda michezo minne ya kwanza, lakini akafuatiwa na droo kabla ya kuchapwa mabao 2-0 na wapinzani wao timu ya Al Ahly kwa mabao 2-0.

Kupoteza katika mchezo huo wa jana kumeifanya Zamalek kuwa nyuma ya Al Ahly kwa jumla ya point 7 katika msimamo wa ligi hiyo.
Mbali na Mido, klabu hiyo pia imemtimua kazi mkurugenzi wake mpya wa soka aliyeajiriwa siku moja na Mido Hazem Emam.

Mido aliyechukua nafasi hiyo kutoka kwa mbrazil Marcos Paqueta anakuwa ni kocha wa tatu kuajiriwa na kufukuzwa na klabu hiyo ndani ya msimu huu na sasa nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Salah ambaye anakuwa kocha wa muda wa klabu hiyo.