Baadhi ya wachezaji wa timu z soka za sekondari nchini wakichuana katika soka.
Michuano ya timu za shule za sekondari nchini kuwania nafasi ya timu za shule kuwakilisha Tanzania katika michuano ya shule za sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki FEASA inayotaraji kuanza August 22, mwaka huu jijini Dar es salaam, imeendelea tena hii leo katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari ya makongo na Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam
Katibu mkuu wa kamati ya maandalizi ya michuano ya FEASA Aaron Sokoni amesema mashindano hayo yatashirikisha shule na hakutakuwa na kombaini ya wachezaji nyota, na ni kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo.
Aidha Sokoni amesema Tanzania katika soka itawakilishwa na timu 4 huku michezo mingine ikitoa timu 3 tatu kwa kila mchezo
Aidha Sokoni amesema michezo ya Rugby, mpira wa magongo, kuogelea, badmnton haitashindaniwa katika michuano ya Tanzania na badala yake Shule za sekondari zenye michezo hiyo zitawakilisha Tanzania moja kwa moja.