Thursday , 25th Oct , 2018

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limethibitisha kufanya malipo kwa klabu zilizoshiriki katika michuano ya klabu bingwa ulaya na michuano ya 'Europa League' msimu uliopita.

Real Madrid wakishangilia ubingwa

Katika mgawanyo huo, Real Madrid na Liverpool ambazo zilicheza fainali mwezi Mei, zimevuna zaidi ya Euro 80 milioni ambazo ni takribani Sh 209 bilioni za kitanzania.

Kwa upande wa Liverpool, imevuna Euro 11 milioni kwa kutinga fainali huku ikivuna jumla ya Euro 81.2 milioni. Real Madrid ikinyakua kitita cha Euro 15 milioni kwa kushinda fainali hiyo kwa mabao 3-1 mbele ya Liverpool, huku kiasi cha jumla ilichovuna katika mashindano ni Euro 88 milioni.

Katika michuano ya 'Europa League', mabingwa Atletico Madrid wameambulia Euro 31.7 milioni ambazo ni sawa na takribani 82.5 bilioni za kitanzania ikiwa ni pamoja na zawadi ya kushinda taji.

Kila klabu ambayo ilifuzu katika hatua ya makundi ya michuano hiyo imeambulia kiasi cha Euro 12.7 milioni. Kwa ujumla, UEFA imelipa jumla ya Euro 1.412 bilioni kwa klabu zilizoshiriki klabu bingwa ulaya, huku ilipa kiasi cha Euro 428.1 milioni kwa klabu ambazo zilishiriki michuano ya Europa League.