Friday , 27th Jan , 2017

Kuelekea katika mchezo wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara utakaowakutanisha wekundu wa Msimbazi Simba SC dhidi ya Azam FC siku ya kesho Simba SC wamesema, mchezo huo siyo kisasi au upinzani kama mashabiki wengi wanavyofikiria.

Mechi ya Simba na Azam katika fainali ya Kombe la Mapinduzi ambapo Azam iliifunga Simba bao 1-0

 

Meneja wa Simba SC Mussa Hassan Mgosi amesema, mpira hauna historia kwani maandalizi ni kwajaili ya mchezo husika na kikosi kimejipanga kwa ajili ya kupambana ili kuweza kuibuka na pointi tatu ambazo zitawaweka katika mbio za kuendelea kuwania Ubingwa wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Mgosi amesema, wameangalia na kuyarekebisha mapungufu waliyonayo ili yasiweze kujitokeza tena katika mchezo ujao ili kujihakikishia kuwa wanaibuka na ushindi ambao ndiyo lengo lao.

Kuhusu hali ya wachezaji Mgosi amesema, wachezaji wote ni wazima na wanasubiri muda wa kocha kuweza kuchagua wachezaji ambao wataingia kupambana katika mchezo dhidi ya Azam FC.

Mussa Hassa 'Mgosi' - Meneja wa Simba

Mgosi amewataka mashabiki wa Simba SC kuendelea kuwapa sapoti ikiwa ni pamoja na kuwa makini katika mechi mbalimbali ili kuendelea kuwa pamoja na kutimiza malengo waliyojiwekea.

Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi, Simba ilishinda bao 1-0, lakini katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi, Azam walilipa kisasi kwa kuifunga Simba bao 1-0, Je kesho itakuwa ni zamu ya nani?