Thursday , 16th Apr , 2015

Mbio za kulaani na kupinga mauaji na ukataji wa viungo vya albino zinatarajiwa kufanyika Aprili 19 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Msemaji wa mbio hizo, Maulid Kisoma amesema, mbio hizo zitakuwa ni zile za polepole yaani Jogging za kilomita tano ambapo viongozi mbalimbali na wananchi kutoka mkoa wa Dar es salaam wanatarajiwa kushiriki katika kufikisha ujumbe huo kwa jamii.

Kisoma amesema mbio hizo zitakuwa endelevu na wanatarajia kuanza na mikoa minne ambayo ni Mwanza, Shinyanga na Mbeya huku wakitarajia kueneza ujumbe huo nchi nzima.