Monday , 12th Sep , 2016

Mauzo ya tiketi katika michezo ya walemavu ya paralimpiki yamefikia milioni 1.8 hivi sasa na kufanya michezo hiyo kuwa ya pili kwa mahudhurio makubwa katika historia.

Baadhi ya mashabiki wakifuatilia uzinduzi wa mashindano ya Paralimpiki

Mwishoni mwa wiki watu wengi walinunua katika kituo cha michezo hiyo, si zaidi ya wiki mbili baada ya waandaji kutangaza kupunguza bei kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi iliyosababishwa na mauzo mabaya ya tiketi.

Kuongezeka kwa mauzo kumetokana na bei nafuu na matangazo.