
Katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mabao ya Deus Kaseke na Amis Tmbwe aliyefunga mawili yakaipa ushindi mabingwa watetezi Yanga wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji ya mkoani Ruvuma.
Nako Jijini Mbeya klabu ya Mbeya City ikaonja kipigo cha kwanza katika ligi msimu huu kufuatia kukubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa wanalambalamba wa Azam Fc ambapo .
Mkoani shinyanga katika uwanja wa Mwadui Comlex wenyeji Mwadui Fc wakalazimishwa sare wakiwa nyumbani dhidi ya nduguzao klabu ya Stand United ya kufungana bao 2-2.
Masarenge wa Ruvu Shooting wakawacharaza wenzao wa Jkt Ruvu katika mchezo uliopigwa kunako uwanja wa mabatini mkoani Pwani nayo Ndanda Fc ikashindwa kutamba katika uwanja wake wa Nangwanda Sijaona baada ya kutoka suluhu na wakatamiwa wa Kagera Sugar.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mitanange miwili ambapo kunako dimba la uhuru wekundu wa msimbazi Simba itawaalika wakatamiwa wa Mtibwa Sugar nayo Tanzania Prisons itaendelea kusalia nyumbani kunako dimba la sokoine jijini Mbeya kuikaribisha Toto Africans ya Mwanza