Monday , 8th Jun , 2015

Mashindano ya majeshi hapa nchini yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho jijini Dar es salaam kwa kushirikisha wanamichezo zaidi ya 1,000 yakiwa na lengo la kutafuta timu ya jeshi itakayoshiriki michezo ya majeshi ya Afrika Mashariki.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Mnadhimu wa Michezo Makao makuu ya Jeshi, Luteni Kanali, Joseph Bakari, amesema, michezo hiyo ni ya hatua ya mwanzo kwa ajili ya kuteua timu bora itakayoshiriki mashindano ya majeshi ya Mashariki.

Luteni Kanali Bakari amesema, mashindano hayo yatakayoshirikisha michezo ya mpira wa miguu wanaume, Netiboli kwa wanawake, Mpira wa mikono kwa wanaume, Mpira wa kikapu kwa wanaume na riadha kwa wanawake na wanaume yatasaidia kupata wanamichezo 100 watakaoshiriki mashindano hayo.