Masau Bwire
Masau Bwire amesema kitendo kilichofanywa na mashabiki wa Yanga sio cha kiungwana ndio maana alifikia uamzi wa kuitoa silaha ili isiibiwe haswa baada ya kuporwa simu ya mkononi aina ya Nokia E71.
''Sikutoa silaha kwa nia ya kumdhuru yeyote lakini iliniladhimu kuihamisha ili isiibiwe kama ilivyoibiwa simu yangu yenye thamani ya dola 310 hivyo sikuwa salama kabisa kwa vitendo vya mashabiki hao ambao sio waungwana'', amesema Bwire.
Aidha Masau Bwire ameweka wazi kuwa mapema leo asubuhi Desemba 17, 2018 ameripoti tukio hilo la kuzongwa na mashabiki pamoja na kuibiwa na simu yake ili taratibu za kisheria ziendelee.
Katika mchezo huo uliopigwa jana Desemba 16, 2018 Ruvu Shooting ilifungwa mabao 3-2 na Yanga hivyo Yanga kufikisha alama 44 kileleni wakiwa wamecheza mechi 16. Ruvu Shooting wao wamebaki kwenye nafasi ya 16, wakiwa na alama 17.



