Friday , 5th Aug , 2016

Bondia wa ngumi Manny Pacquiao ametangaza kurejea ulingoni tarehe 5 Novemba kupambana na bingwa wa dunia wa uzani wa welter, Jessie Vargas kutoka Marekani.

Bondia wa ngumi Manny Pacquiao

Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 na bingwa wa zamani wa dunia, ametangaza kwamba atarejea tena kwenye ndondi licha ya kutangaza kwamba angestaafu baada ya kumshinda Timothy Bradley mwezi Aprili huu.

Aidha, meneja wake Michael Koncz alisema kuwa Manny hawezi kustaafu kwa sasa kwa sababu ndondi ipo kwenye damu yake.

"Maisha ya kustaafu hayamfai Manny kwa sasa, ndondi zimo kwenye damu yake."

Pacquiao na kundi lake watakutana 10 Agosti mjini Manila kuamua iwapo pambano hilo dhidi ya Vargas mwenye umri wa miaka 27 litaandaliwa Los Angeles au Dubai.