
Nembo za Man City na Man United
Manchester City ambayo inaongoza ligi mpaka sasa, ikiendeleza ubora wake tangu msimu uliomalizika ambapo ilifanikiwa kunyakuwa ubingwa, inakutana na Manchester United ambayo imeanza kuimarika katika michezo yake ya karibuni baada ya kupitia kipindi kigumu tangu mwanzo wa msimu.
Katika mchezo wa kwanza msimu uliopita, Man city iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Old Trafford, na katika mchezo wa pili uliochezwa mwezi April katika uwanja wa Etihad, Man United iliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Rekodi ya michezo iliyozikutanisha timu hizo tangu Novemba, 2010 mpaka sasa zinaonesha kuwa Man United imeshinda mara tisa huku Man City nayo ikishinda mara 9 pamoja na michezo sita iliyomalizika kwa sare.
Man City inaongoza ligi kwa jumla ya alama 29 huku Man United ikishika nafasi ya nane kwa alama zake 20 mpaka sasa.