Mwenyekiti wa DAREVA Siraju Mwasha amesema, wanaamini wakiwa na makocha wengi wa mkoa watakuwa na timu zenye makocha wengi ambapo timu zitaweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Mwasha amesema, washiriki wa kozi hiyo ni walimu wa shule za msingi na sekondari ambao wataweza kuufundisha mchezo huo mashuleni kabla ya kuanza zoezi zima la kutafuta wanafunzi watakaounda timu mbalimbali za vijana za mchezo huo jijini Dar es salaam.
Mwasha amesema, baada ya kumaliza kozi hiyo itakayokuwa ya mkoa makocha hao wataendelea na mafunzo ya kitaifa itakayotolewa na waalimu kutoka nje ya nchi ili kuweza kuwapa elimu zaidi juu ya mchezo huo.
Mwasha amesema, kozi hiyo inayoanza Septemba 12 mpaka Septemba 17 itashirikisha makocha takribani 30 kutoka shule mbalimbali jijini Dar es salaam.