Wednesday , 12th Dec , 2018

Kocha wa timu ya Kikapu ya San Antonio Spurs, Gregg Popovich ameingia kwenye rekodi za ligi ya kikapu nchini Marekani, baada ya kuwa kocha wa nne kati ya watano walioshinda mechi nyingi zaidi katika ligi hiyo.

Kocha wa San Antonio Spurs, Gregg Popovich.

Gregg Popovich alikabidhiwa kijiti cha ukocha mkuu wa San Antonio Spurs mwaka 1996 akitokea Golden State Warriors ambayo alikuwa kocha msaidizi chini ya Don Nelson kuanzia mwaka mwaka 1994.

Gregg Popovich  ambaye sasa ameshinda mechi 1211, pia yupo kwenye orodha ya makocha walioshinda mataji mengi katika ligi ya kikapu ya NBA akiwa ameweka kabatini mataji matano yote akiwa na timu ya San Antonio Spurs.

Orodha kamili ya makocha
1. Don Nelson ameshinda mechi 1335.
2. Lenny Wilkens ameshinda mechi 1332
3. Jerry Sloan ameshinda mechi 1221
4. Gregg Popovich ameshinda mechi 1211
5. Pat Riley ameshinda mechi 1210

Don Nelson alifundisha timu za Milwaukee Bucks, New York Knicks, Dallas Mavericks na Golden State Warriors. Lenny Wilkens alifundisha Seattle super Sonics (Oklahoma City thunder) Portland Trail Blazers na nyingine.