Manahodha wa timu zinazocheza nusu fainali ya pili michuano ya Sprite BBall Kings.
ofisi za EATV LTD mchana wa leo.
Nahodha wa timu ya Flying Dribblers, Geofrey Lea amesema hawezi kuzungumzia kwa sasa sababu ya wao kufungwa katika mechi yao ya kwanza na wapinzani wao Mchenga BBall Stars na kudai wameshaanza kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza siku hiyo.
"Wenzetu walishinda tunawapongeza kwa hilo, walikuwa bora zaidi yetu. Nisingependa kuzungumzia sana sababu ya kwanini tulipoteza mchezo wa kwanza kwa kuwa hazina msingi sana ila kikubwa tumeelewa mapungufu yetu yaliyojitokeza na tumekuwa tukiyafanyia kazi kwa muda wa siku zote hizo. Kwa hiyo matumaini yetu ni makubwa sana tutahakikisha kwamba tunafia uwanjani ili ku-force 'game three' kwa mechi ijayo", amesema Geofrey Lea.
Makocha wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu.
Kwa upande wake Nahodha wa Mchenga BBall Stars, Mohamed Yusuph amesema wataendelea na mapambano yao ili wahakikishe wanakuwa washindi katika michuano hiyo itakayoendelea kuchezwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya Don Bosco Oyster Bay Jijini Dar es Salaam.
"Timu tuliyokutana nayo katika nusu fainali siyo timu rahisi kama watu wanavyofikilia kwa kuwa na wao walipambana hadi mwisho kufikia katika hatua hii. Kama wao walivyosema kwamba wamejipanga katika ku-force kucheza mechi ya tatu basi 'okey' kama kuna 'business' tutafanya na kama hakuna 'game 2 itakuwa 'end' tunamaliza", amesema Mohamed.
Kwa upande mwingine, timu zote zinazoshiriki kwenye michuano hiyo katika nyakati tofauti zimedai wakipata zawadi ya mshindi wa kwanza yenye thamani ya Milioni 10 za kitanzania basi wataweza kurudisha shukra zao kwa jamiii huku wengine wakisema wataanzisha timu za watoto ili kusudi waweze kuujenga zaidi mchezo wa mpira wa kikapu.