Sunday , 15th Mar , 2015

Wadau mbalimbali wa mchezo wa soka wakiwemo ndugu jamaa na marafiki wamejitokeza leo kumuaga Kocha Sylvester Marsh katika safari yake ya mwisho.

Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania taifastars marehemu Silvester Marsh.

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Sylvestre Marsh, ameagwa leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Marsh aliyefariki dunia jana, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua maradhi ya saratani ya koo kwa muda mrefu.

Awali alilazwa hapo akapata nafuu na kupelekwa kwao Mwanza, lakini wiki iliyopita alirudishwa tena na ndipo umauti ulipomkuta.

Mwili wa Marsh umesafirishwa leo kwa njia ya barabara kuelekea Igoma mkoani Mwanza ambapo maziko yatafanyika

Wakizungumza hii wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Marsh ambaye aliwahi kufundisha taifa stars katika vipindi tofauti akiwa na makocha Mbrazil Marcio Maximo pamoja na wadernmak Jan Palsen na Kim Palsen makocha Meck Mexime ambaye aliwahi kufundishwa na kocha huyo pamoja na mwalimu wa marehemu kocha Rogasian Kaijage wamesema marehemu Marsh ameacha pengo na yale mazuri yote yaliyofanywa na marehemu kocha Marsh yapaswa kuendelezwa hasa ukuzaji soka kwa vijana wadogo

Kwa upande mwingine kufuatia mwili wa Marsh kusafirishwa jioni hii kwa njia ya barabara kuelekea mkoani Mwanza kwa mazishi mmoja wa mashabiki wakubwa wa timu ay taifa Stars Ally Yanga amekisikitikia kutokana na makubwa aliyofanya kocha huyo akidai hakupaswa kusafirishwa katika hali hiyo na hivyo kulitaka shirikisho la soka kuthamini wanamichezo waliofanya makubwa katika soka hapa nchini hasa ukichukulia mtu kama Marsh alikua na timu ya taifa stars kwa miaka takriban 10