Luol Deng
Deng mwenye umri wa miaka 31, ambaye anacheza nafasi ya ushambuliaji, alikuwa na wastan wa pointi 12.3 katika michezo 74 alizoichezea Miami Heat msimu uliopita, tangu kujiunga na timu hiyo mwaka 2014.
Muingereza huyo ambaye ni mzaliwa wa Sudan, aliiwakilisha Uingereza katika kikosi chake cha Olympic ya mwaka 2014 pia amewahi kuichezea Chacago Bulls mwaka 2004 hadi 2014.
Wakati Deng akielekea Lakers, mwenzake Dwyane Wade ambaye aliibuka katika kikosi NBA All-Star mara 12, anaondoka Miami na kujiunga na Chicago.
Wade ambaye anacheza nafasi ya ulinzi, amekubali mkataba wa miaka miwili kwa dau la dola za kimarekani milioni 47.5 (Zaidi ya shilingi bilioni 90 za kitanzania)
Wade mwenye umri wa miaka 34 ameelezea furaha yake kujiunga na Chicago na kusema kuwa hapo ni nyumbani kwake, na anajisikia furaha kurudi nyumbani ambapo amekulia.




