Monday , 7th Nov , 2016

Shirikisho la Soka nchini TFF limesimamisha ligi ya Wanawake iliyotarajiwa kuendelea tena hapo kesho ili kupisha mchezo wa kirafiki wa timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars itakayopambana na Cameroon katika mchezo utakaopigwa Novemba 10, Cameroon

Kilimanjaro Qeens

Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema, ligi hiyo ilitakiwa kuendelea kesho lakini utapigwa mchezo mmoja pekee ambao ni Panama dhidi ya Marsh Academy ya Mwanza huku Twiga ikiwa tayari kambini na inatarajiwa kuondoka hapo kesho kuelekea nchini Cameroon kwa ajili ya mchezo huo.

Lucas amesema, mchezo wa Panama dhidi ya Marsh Academy ulipangwa kupigwa mara baada ya Twiga kumaliza mchezo dhidi ya Cameroon lakini kutokana na Panama kuwa tayari imeshawasili Mwanza wameamua mchezo huo uchezwe.