Thursday , 8th Dec , 2016

Vilabu 10 vya shule za sekondari kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar vinataraji kushiriki katika shindano maalum la taifa la mchezo wa Baseball na Softball itakayofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 9 mwaka huu.

Wachezaji wa mchezo wa Baseball wakichuana.

 

Katibu mkuu wa Chama cha Baseball na Softball Tanzania TABSA Alpherio Nchimbi amesema hayo wakati akizungumza na kipindi cha Kipenga juu ya maandalizi ya michuano hiyo ambayo pia itahudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wa mchezo huo duniani.