Thursday , 9th Apr , 2015

Ligi ya kikapu klabu bingwa taifa ya wanawake inatarajia kuanza kutimua vumbi Aprili 12 mpaka 17 mwaka huu, uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Kamishna wa Ufundi na uendeshaji wa mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini TBF, Manase Zabroni amesema, lengo hasa la kuanzisha michuano hiyo ni kuweza kukuza mchezo huo kwa upande wa wanawake ili kuweza kushiriki katika mashindano makubwa ndani na nje ya nchi.

Manase amesema, pamoja na yote pia wanatarajia kushirikisha timu ya Mpira wa kikapu kwa wanawake katika Mashindano ya UMISETA na UMITASHUMTA kwa mara ya kwanza.