Sunday , 26th Oct , 2014

Katika muendelezo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es salaam BD, mashabiki wa mchezo huo wamesema hivi sasa timu nyingi zimejiandaa kwa ajili ya ligi hiyo ambayo imezidi kukua kwa kasi hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, mmoja wa mashabiki wa mchezo huo, Mopelle Mubarack amesema timu nyingi zimejitoa kutokana na kila mechi kuwa na ushindani kutokana na kila timu kujiandaa ambapo pia imepelekea timu kuongezeka katika mchezo huo.

Mubarack amesema wadhamini wanatakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuutangaza mchezo huu na kuweza kuukuza zaidi ndani na nje ya nchi.

Tags: