Thursday , 23rd Apr , 2015

Ligi kuu Soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea hapo kesho kwa mchezo mmoja ambapo utawakutanisha Ruvu Shooting ikiwakaribisha Yanga Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema, mchezo ni dakika tisini na matokeo yote yatapatikana ndani ya dakika hizo.

Bwire amesema, katika mechi hiyo wachezaji watathibitisha kiwango walichonacho katika kucheza mpira.

Yanga inaingia katika mchezo huo ikiongoza katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa kuwa na Pointi 49 huku mafande wa Ruvu Shooting wakiwa na Pointi 29.