
Akizungumza jijini dar es salaam, Afisa Habri wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania TFF, Baraka Kizuguyto amesema, Katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi Morogoro watawakaribisha maafande wa Ruvu Shooting kutoka Mlandizi huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa Kagera Sugar kwenye dimba la Mkwakwani jijini Tanga ambapo JKT Ruvu wakiwa ugenini kucheza na Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Azam FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es salaam.
Kizuguto amesema, Jumapili Mgambo JKT watakua wenyeji wa timu ya Ndanda FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Mtibwa Sugar wakiwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika Uwanja wa Manungu Turiani.
Kizuguto amesema, Katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watani wa jadi Simba SC watakuwa wenyeji wa Young Africans, mchezo unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.