Ni katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba wanashuka dimbani wakiwa kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zao 45 baada ya kucheza mechi 19, wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 43 za mechi 18.
Hiyo inamaanisha mchezo huo wa watani wa jadi ndiyo utaamua timu ya kutakaa kileleni baada ya mechi za mzunguko wa 20.
Simba imekuwa kambini Chuo cha Biblia eneo la Bigwa mkoani Morogoro tangu Jumapili ikitokea mkoani Shinyanga ambako ilishinda mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu, wakati Yanga ilikuwa kisiwani Pemba, ambako iliwasili Jumapili ikitokea Mauritius. Ni Yanga tena, au Simba leo Uwanja wa Taifa? Dakika 90 zitatoa majibu.



