Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu nchini TAVA, Augustino Agapa amesema, lengo hasa la kozi hiyo ni kuweza kupata maalimu watakaoweza kutoa mafunzo ya mchezo huo kwa watoto na kuwajenga ili baadae waweze kupata timu ya taifa ya mchezo huo.
Agapa amesema, Kozi hiyo itaendeshwa na Kocha wa mchezo huo kutoka nchini Ujerumani ambapo anatarajiwa kuwasili nchini April Nane kwa ajili ya kukagua uwanja pamoja na ukumbi wa kutolea mafunzo hayo.