Pambano hilo litasimamiwa na PST ambapo rais wake Emmanuel Mlundwa amewataka mabondia hao kucheza mchezo uzuri katika pambano hilo ambalo amesema litakua la raundi 10 kuwania mkanda wa kimataifa wa UBO Afrika
Nao mabondia hao Japhet Kaseba na Thomas Mashali ambao wamevuta hisia kwa mashabiki wao mara baada ya zoezi la upimaji uzito kila mmoja ameatamba kuibuka na ushindi na kuwataka mashabiki wao wasiwe na wasiwasi juu ya pambano hilo
Na katika kuhakikisha mpambano huo unakuwa na maamuzi ya haki na usawa katika maamuzi ya mapambano yote hapo kesho, Mratibu wa pambano hilo Ramadhan Mwazowa ametoa wito kwa majaji na waamuzi wa mchezo huo kuchezesha na kuwa na maamuzi yatakayozingatia sheria za mchezo huo
Mwazowa ameongeza kuwa uchezeshaji unaozingatia sheria na taratibu za mchezo huo kimataifa utafungua milango kwa waamuzi hao kupata michezo mingi ya kimataifa nje ya nchi.