Thursday , 29th May , 2014

Kaseba amesema dawa pekee ya kuzima maonezi katika maamuzi ya mapambano ambayo yanaamuliwa kwa pointi za majaji ni kuwapiga mabondia anaokutana nao kwa pigo la Knock out na ulaya ndio sehemu pekee atakapo[ta dawa hiyo

Bondia Japhet Kaseba akiwa katika mazoezi.

Bondia Japhet Kaseba yuko katika mazoezi mazito akijifua kwa ajili ya safari ya kwenda katika ziara ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi barani Ulaya.

Kaseba amesema amelazimika kwenda katika mafunzo hayo ili kujiongezea ufundi zaidi katika masumbwi kwa lengo la kutaka kushinda kwa knock out mapambano yake.

Kaseba amesema kwakuwa mapambano mengi aliyocheza na mabondia wakongwe hapa nchini ambayo yaliamuliwa kwa pointi ambapo yeye anasema alikuwa hatendewi haki na mara nyingi mabondia hao walikuwa wanabebwa na hivyo pigo pekee la kuondoa utata ni kupiga pigo la knock out tu.