Saturday , 22nd Mar , 2014

Bondia Japhet Kaseba yuko katika maandalizi mazito ya mwisho mwisho akijifua tayari kwa mpambano

Bondia Japhet Kaseba yuko katika maandalizi mazito ya mwisho mwisho akijifua tayari kwa mpambano wa ubingwa wa UBO dhidi ya bondia Thomas Mashali mpambano utakaopigwa machi 29 mwaka huu katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam.

Kaseba ambaye anajifua katika gym yake maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es salaam amesema kuwa kutokana na muda wa mpambano huo kukaribia, hivi sasa anafanya mazoezi mepesi ili kujiweka fiti na amewahakikishia mashabiki wake kwamba atamtwanga Mashali siku hiyo na kutwaa mkanda huo japo anajua mpambano huo utakua mgumu mno hasa kutokana na ubora na uzoefu wa mpinzania wake Mashali.