Friday , 5th Aug , 2016

Beki kisiki wa kulia wa Azam FC Shomari Kapombe, ameandaliwa dakika maalum za kucheza kwenye mechi za kujipimba nguvu, ili kurejea kuwa fit, baada ya kuumwa kwa miezi 4.

Mtaalamu wa Viungo wa Azam FC, Sergio Perez Soto, amesema Mlinzi wa kulia wa timu hiyo Shomari Kapombe yuko fiti kwa sasa na anachojaribu kukifanyia kazi ni kumpa dakika chache za kucheza ili kutathimini kiujumla maendeleo yake.

BAADA ya kukosekana uwanjani kwa muda wa siku 122 (sawa na miezi minne), beki Kapombe, amecheza mechi yake ya kwanza tokea apone wakati Azam wakilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya JKT Ruvu siku ya jumatano.

Soto, amesema, anatarajia kuendelea kumwangalia na anaweza kupewa dakika 30 katika mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting),lengo likiwa ni kuona anakuwemo kwenye mchezo dhidi ya Yanga (Agosti 17).