Kiungo Mzimbabwe,Thabani Scara Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara kwa mwezi Desemba 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga SC Mrundi Amissi Tambwe.
Kamusoko ameisaidia timu yake ya Yanga katika michezo iliyochezwa Desemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo minne iliyochezwa mwezi huo wa mwisho wa mwaka.
Kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi Disemba, Kamusoko atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu.
Kamusoko na Donald Ngoma ni Wazimbwabwe waliosajiliwa na Yanga msimu huu wakitokea klabu ya Platinum ya nchini Zimbabwe.



