Sunday , 23rd Aug , 2015

Beki wa zamani wa Klabu ya Simba anayeitumikia timu ya Neckarsulmer Emily Mgeta,amesema anaamini juhudi aliyonayo katika mechi mbalimbali dhidi ya timu yake hiyo vitamfikisha mbali zaidi katika soka na kuendelea kuitangaza Tanzania kwa upande wa soka

Katika taarifa yake, Mgeta amesema, katika mchezo waliocheza hapo dhidi ya Heiningen wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 suala linalozidi kumpa moyo wa kuzidi kujipa moyo wa kuendelea kusonga mbele zaidi.

Mgeta amesema, ameichezea timu yake kwa dakika 70 ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza Ligi ya Ujerumani inayotambulika kama Verbandsliga ambapo kikosi chake kilikuwa ugenini lakini kilifanikiwa kufunga bao kila kipindi.