Thursday , 12th Feb , 2015

Washiriki wa michuano ya Judo kanda ya tano wanatarajia kuanza kupima uzito hapo kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 14 mpaka 15 Mjini Moshi kwa kushirikisha nchi saba.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu mwenyekiti wa Chama cha Judo nchini JATA, Mgowe Omary amesema, michuano hiyo inayotarajia kushirikisha uzito wa kuanzia kilo 60 hadi 100 itashirikisha nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Zanzibar, Rwanda, Ethiopia pamoja na wenyeji Tanzania na nchi zote zimeshawasili kwa ajili ya michuano hiyo.

Mgowe amesema, baada ya kupima uzito, kutakuwa na kikao cha viongozi wa ukanda huo, semina kwa waamuzi pamoja na ukaguzi wa wachezaji kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Timu ya Taifa ya Tanzania ambao ndiyo wenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka huu, ilinyakua ubingwa huo katika mashindano yaliyofanyika Nairobi, Kenya na mwaka 2013 yalipofanyika Visiwani Zanzibar.