Monday , 25th May , 2015

Katika kujiimarisha mapema kabla ya msimu ujao wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara, Timu ya JKT Ruvu imepanga kuingia kambini Julai 22 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Habari wa timu hiyo, Costantine Masanja amesema, wamewapa wachezaji wao likizo ya mwezi mmoja kwa ajili ya kupumzika lakini wanaingia kambini mapema ili kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kujiandaa na ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.

Masanja amesema, katika msimu uliopita hawakufanya vizuri lakini wanaamini msimu ujao watafanya vizuri kwani mazoezi yataanza mapema ikiwa ni pamoja na kuwapima wachezaji ambao wapo nao kwa ajili ya majaribio.

Masanja amesema, kocha Fredy Minziro ameshakabidhi ripoti yake na sasa wapo katika mikakati ya kuitekeleza.